MADIWANI HALMASHAURI
YA WILAYA YA NZEGA MKOANI TABORA WAMPONGEZA RAIS SAMIA.
MADIWANI HALMASHAURI
YA WILAYA YA NZEGA MKOANI TABORA WAMPONGEZA RAIS SAMIA.
Na Odace Rwimo Nzega
MADIWANI wa
halmashauri ya Wialaya ya Nzega wametoa
tamko la pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu
Hassan kwa kuimwagia mabilioni ya fedha halmashauri hiyo ili kufanikisha
utekelezaji miradi ya kimkakati.
Akitoa tamko hilo
mwenyekiti wa Halmashauri yaWilaya ya Nzega Henrico Kanoga ,alisema Rais amegusa
mioyo ya wakazi wa wilaya hiyo kwa
kuwapatia fedha nyingi ili kutekeleza miradi yenye maslahi mapana kwa wananchi.
Alibainisha kuwa
Mheshimiwa Rais ana dhamira njema ya kuinua maisha ya wananchi ndiyo maana
ameendelea kupeleka fedha nyingi katika halmashauri zote nchini ikiwemo
Halmashauri ya Nzega ili kuhakikisha huduma bora za kijamii
zinapatikana wakati wote.
Alitaja baadhi ya
sekta ambazo zimepokea fedha katika halmashauri hiyo kwa ajili ya utekelezaji
miradi ya kimkakati kuwa ni elimu, maji, afya na miundombinu ya barabara.
Kanoga alibainisha kuwa hivi karibuni tu wamepokea
kiasi cha zaidi ya sh bil 2 kwa ajili ya
miradi ya elimu lengo likiwa kuifanyia maboresho makubwa miundombinu ya shule
za msingi na sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya nzega.
Kwa upande wake
mkugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nzega Eng.Modest Aporlinary aliwataka wakuu
wa vitengo na idara ndani ya halimashauri kila mmoja kusimama katika nafasi ili
kutimiza kusudio la Mh.Rais.
Alisema endapo kila
mtumishi wa umma ataweza kutimiza wajibu wake kwa asilimia 100 watamsaidia Rais
kutimiza nia nzuri aliyonayo hasa katika kuboresha miundombinu ya elimu,afya na
Barabara.
“Unajua katika halmashauri yangu ninayo miradi
mingi ambayo ipo inatekelezwa tukianzia mradi wa ujenzi wa makao makuu ya
Halmashauri mradi unaogharimu zaidi ya bilioni 1.8, kuna miradi ya boost
katika shule zetu za msingi nayo inayoendelea kujengwa pamoja na madarasa na vyoo katika shule za
sekondari,tusiposimamia kwa uzalendo tunaweza kufuta nia ya rais kwa wananchi
wake.”alisema Apolinary
Alisema kwa dhamana niliyopewa na Mh.rais ya
kusimamia miradi ya maendeleo na watumishi wa halmashauri hii sitofumbia macho
mtumishi mwenye nia ovo ya kuharibu ama kutumia madaraka yake vibaya kwa
kutofuata sheria na kanuni za kazi.
Aidha baadhi wa madawani nao wakachangia hoja
kwa kumtaka mkurugenzi kusimamia mapato ya ndani ili kuweza kukidhi bajeti
inatekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 pamoja na bajeti ya mwaka 2023/2024
kwani ndio itakayosaidia kuchangia miradi mingine ya maendeleo.
Akizungumza
kwa niaba ya madiwani wenzake diwani waka kata ya Lusu Said Mgalula
alisema wanampongeza Rais Samia kwa kazi
nzuri inayoifanya ya kulijenga taifa lenye maendeleo kuanzia ngazi ya kijiji
mpaka taifa.
Alisema wanajivunia saana kazi nzuri
inayofanywa na serikali ya awamu sita kwani wamefika maeneo yote yanayogusa
maisha ya watu hasa katika Nyanja za elimu na Afya hakika ameupiga mwingi
anahitaji maua yake.