Afisa tawala Wilaya ya Nzega Mkaoni Tabora Amina Matua akiwa na Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Boaz Mwaikugile wakiwa kwenye kikao cha Lishe.
Na Odace Rwimo,Nzega DC.
Suala la lishe limekuwa ni suala mtambuka katika
jamii hali inayochangia udumavu kwa watoto kuanzia miaka 0-5 huku kwa watu
wazima nao wakikumbana na na hali ya lishe duni.
Katika kutekeleza mkataba wa lishe kwenye kata za
Halmashauri ya wilaya ya Nzega Mkoani tabora kwa kipindi cha july-september
idara ya afya imeweka mpango kazi wa kuhakikisha wanazifikia shule za msingi na
sekondari pamoja na jamii kwa ujumla.
Akizungumza katika kikao lishe afisa lishe Rahma
Sheshe kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega Mkoani
hapa alisema wameanza mkakati wa kukutana na wadau mbalimbali ili kuweza kutoa
elimu juu ya umuhimu wa lishe bora kwa kila mtu.
Alisema kumekuwepo na matatizo mengi katika jamii
ambayo yanasababishwa na lishe duni hasa kwa kutozingatia masuala ya chakula
kipi kinatakiwa kuliwa kwa wakati upi na mda gani hali ambayo imekuwa ni tatizo
kwa jamii.
“Tunapozungumzia suala la lishe si kwa watoto tu
bali hata watu wazima wanatakiwa kuzingatia lishe kwa ujumla ili kujenga miili
yenye afya na nguvu wakati wote kwani ukiangalia vijana wengi wamekumbwa na
tatizo la nguvu za kiume kutokana na lishe duni”
Alisema Idara ya lishe kushirikiana na idara ya maendeleo ya jamii kuhamasisha tayari wameanzisha mpango kazi wa kutembelea baadhi ya maduka
kwa ajili ya kuangalia utunzaji wa vyakula sanjari na kuhamasisha ulimaji
chakula katika mashamba ya shule.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa halmashauri ya
Wilaya ya Nzega Dr.Boaz Mwaikugile alisema wao kama halmashauri tayari wameisha
andaa mikakati ya kuhakiksha lishe inazingatiwa kwa kila mtu hasa kwa watoto wa
shule na kutoa elimu kwa kila mwananchi juu ya umuhimu wa lishe.
Alisema jambo la kwanza ni kuhakikisha kwanza
wanatunga na kuweka wazi sheria ndogondogo zitakazo wabana wazazi/walezi
wanaogoma kuchangia chakula.
Wananchi wa kata ya Lusu wilayani Nzega wakiwa kwenye kikao cha lishe kilichofanyika hivi karibuni katani hapo ikiwa ni siku ya Lishe Duniani.
Alieleza kuwa wanaandaa utaratibu mzuri kwa shule
zinazolima vyakula zikopeshwe mbolea kulingana na ukubwa wa maeneo yao
wanayolima kwa kuwa ardhi nyingi zimechoka hivyo kupelekea mavuno kidogo.
Aidha Dr.Mwaikugile aliomba wakuu wa idara kufanya
vikao na wanasiasa kuwa elimisha kutoingilia mamuzi ya kuwachangisha vyakula
wazazi pamoja na walezi ili kuweza kufanya shule nyingi kuwapatia watoto
chakula wawapo shuleni.
Hata hivyo afisa tawala wilaya ya Nzega Amina Matua kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai alisema kuna kila sababu ya kutoa elimu na kuhamasisha upatikanaji wa chakula shuleni kuanzia shule za msingi na sekondari.
Alimtaka afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya
ahakikishe anaandaa na kufanya mikutano na makongamano ya mara kwa mara
kuhamasisha suala la lishe ili kunusuru udumavu kwa watoto na changamoto za
kiafya kwa watu wenye umri mkubwa.
Alisema endapo halmashauri itaweka mikakati
iliyoimara itafanikishwa suala la uimalishaji wa lishe katika jamii itasaidia
kutoa elimu kwa wale ambao wamekuwa hatilii mkazo suala la umuhimu wa lishe.