Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya akikagua moja ya gari linalotengenezwa katika Karakana ya Wakala wa Ufundi na umeme (TEMESA) Tabora.
Na Lucas Raphael,Tabora
TANROADS WATAKIWA KUJIPANGA MVUA ZA VULI
Mameneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Wametawakiwa kuhakikisha barabara kuu na za mikoa nchini kote hasa sehemu za korofi, mitaro na madaraja yanasafishwa na kuimarishwa ili kukabiliana changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua za vuli zinazotarajiwa kuanza kunyesha msimu huu wa masika.
Raia hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya alipokuwa akikangua maendeleo ya ujenzi wa Barabara ya Tabora-Mambali-Bukene ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea katika maeneo korofi kabla ya mvua kuanza kunyesha .
Alisema kwamba kipindi cha masika barabara nyingi zimekuwa zinakata wamawsiliaono na zingine kuharibika kutoakana na kutochukua taadhari na kuziona mvua ni kidogo .
Naibu Waziri Mhandisi Kasekenya alisema upo umuhimu wa wajenzi na wasimamizi wa barabara kufuatilia na kufanyia kazi taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA).
“Habari zinasema mvua za vuli zinatarajiwa kunyesha katika kiwango cha juu ya wastani hivyo ili kuepuka mafuriko, kukatika kwa barabara na madaraja ni vema kila meneja katika mkoa wake akajipanga mapema kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza ili kutoathiri huduma za usafiri na uchukuzi”, alisema Mhandisi Kasekenya.
Muonekano wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Vijijini linalojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika kijiji cha lubisu.
Kwa mujibu wa TMA kati ya mwezi Oktoba hadi Disemba maeneo mengi ya mikoa ya Kagera, Geita,Mwanza, Shinyanga, Simiyu,Kigoma, Dar es salaam, Pwani, Morogoro na Tanga yanatarajiwa kupata mvua za juu ya wastani na wastani.
“Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro inatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani hivyo umakini na utayari wa kukabiliana na mvua hizo pale zitakapoleta madhara kwenye miundombinu unahitajika ili kuondoa usumbufu kwa wasafiri”, alisisitiza naibu waziri huyo wa ujenzi.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kasekenya ametoa siku 14 kwa Mtendaji mkuu wa TEMESA kufuatilia ukarabati wa karakana ya TEMESA mkoani Tabora ili kujiridhisha kama unakwenda sambamba na malengo ya Serikali ya kuboresha karakana hizo nchini.
“Tunataka karakana za TEMESA ziwe za kisasa kimuonekano na kwa huduma zinazotolewa ili kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya sita” alisema Mhandisi Kasekenya.