Mratibu wa TASAF Jovitha Kakula akiwa na Afisa ufuatiliaji Irene Shayo kwenye picha ya pamoja na Walegwa wa mpango wa kunusuru Kaya masikini Isagenhe

  TASAF YAINUA FAMILIA MASIKINI

NA ODACE RWIMO, NZEGA DC

Miongoni mwa familia masikini ambazo zinanufaika na mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF nchini hapa zimeanza kunufaika na mpango huo kwa kujipatia maisha mazuri kama watu wengine.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanufaika wa mpango huo ambao mpaka hivi sasa wamejikita katika ujenzi wa nyumba za makazi ya kuishi na kuanzisha miradi mbalimbali kama vile ufugaji na kilimo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini wamesema wameanza kuona mabadiliko makubwa katika maisha yao tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo hata mlo ulikuwa ni mmoja jambo linalokinzana na afya ya binadamu.


Holo Shija mkazi wa kijiji cha Kidete Kata ya Isagenhe akionesha mafanikio aliyoyapata tangu aanze kunufaika na Mpango wa kunusuru kaya masikini

Wanasema kabla ya kujiunga na mpango wa kunusuru kaya masikini hali ya maisha yao ilikuwa ngumu jambo ambalo limesababisha hata watoto wao kutokupata elimu kama watoto wengine jambo ambalo limeathili familia nyingi.

Walisema kufautia kuungwa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini sasa umeanza kusaidia familia zao kubadilika kimaisha ikiwa ni pamoja na kupeleka watoto wao shuleni kupata elimu kama watoto wengine.

Walisema suala la kujenga nyumba za kuisha sasa kwao limeanza kuwa jambo rahisi kwani wanatumia fedha wanazozipata kupitia mpango huo katika kaunzisha ujenzi wa nyumba zao binafsi na kuondokana kuishi yumba za tembe na nyasi.

Masanja Mwagala mlengwa wa mpango wa Kunusuru kaya masikini TASAF katika kijiji Cha Isagenhe akionesha mradi wa ufugaji Kuku.

Mmoja wa wanufaika kutoka katika kijiji cha Kidete Kata ya Isageghe Holo Kanijo alisema maisha yake kabla ya kujiunga na mpango wa kunusuru kaya masikini yalikuwa mabaya na yasiyoelezeka lakini tangu alipopata nafasi kuwa miongoni mwa wanufaika hali imekuwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Alisema kwa sasa wamepata nafasi ya kujiunga katika vikundi na kuanzisha miradi ambayo inasaidia kusukuma maisha yao na kufanya maendeleo mengine ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto wao.

Alisema kupitia mpango wa kunusru kaya masikini anaamini kila atakapo pata malipo ya mwezi atafanya jambo la  maendeleo na kuongeza mradi ambao  utasaidia kukuza kipato cha familia.


Chausiku Muhenda akiwa kwenye shamba la Mihogo pamoja na Afisa ufuatiliaji Irene Shayo ikiwa ni moja ya mradi ambao ameanzisha kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini

Hata hivyo baadhi ya wanufaika kutoka Vijiji vya Isagenhe na Kijiji cha Buhulyu,Masanja Maganga na Pili Mwagala wameishukuru Serikali kwa jinsi ambavyo imeendelea kuwapatia msaada ambao umekuwa ni mkombozi katika familia zao .

Walisema  wanajivunia serikali ya awamu sita kwani inawajali watu wote hata wenye kipato cha chini huku wakibainisha namna ambayo maisha yao yameendelea kuwa bora zaidi kupitia TASAF kwani wameweza kujitegemea na kusomesha watoto ambao mwanzo walikuwa wanakosa haki zao za msingi.

Aidha kwa upande wake Afisa Ufuatiliaji Irene Shayo aliwakumbusha wanufaika wote kutambua haki na wajibu wao ili kuweza kukidhi vigenzo vya kuwa walengwa ikiwa ni pamoja na namna ya kuboresha taarifa zao kila wakati.


Pili Mhoja mnufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini katika kijiji cha Buhulyu kata ya Isagenhe akionesha mafanikio ambayo amepata kupitia mpango huo akiwa na Mbuzi na Kondoo

“Unajua hapa kuna watu hawajui wajibu wao wala hata haki zao za msingi kama mlengwa na mnufaika hivyo mimi Afisa Ufuatiliaji nitakuwa nawatembelea mara kwa mara kuja kuwakumbusha na kuwaelekeza kitu gani mnatakiwa kutimiza kama walengwa”alisema Shayo.

Alisema moja ya kujukumu la kwanza la mlengwa kuboresha taarifa zake za kaya hasa kama kuna mwanakaya ameogozeka,mtoto kahitimu shule ama kuanza shule ya msingi na sekondari au kuna mwanakaya amekosa sifa za kuendelea kuwa kwenye mpango wa kunufaisha kaya masikini na wakati mwingine sababu za kifo.