ISANGA BINGWA MGALULA
CUP
WACHEZAJI WA ISANGA fC WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA KABLA YA KUANZA KWA NTANENGE WA MGALULA CUP.
Na Odace Rwimo
Timu ya Isanga FC
imeibuka bingwa wa Mgalula Cup baada ya
matokeo ya jumla kwa kuongoza katika ushindani wa timu Tatu za Isanga,Ikulu na
Ifumba huku mshindi wa Pili ikiwa ni timu ya Ifumba Ikulu na ikijinyakulia nafasi ya tatu.
Awali diwani wa kata ya
Lusu Said Mgalula alipongeza timu zote ambazo zilishiriki katika mashindano
hayo mpaka kufika tamati kwani michezo ni burudani lakini huwaleta watu sehemu
pamoja.
Alisema ataendelea
kufadhili michezo mbalimbali katika kata yake kwani imekuwa ikileta faida kubwa
hasa ya kuwaunganisha watu wa kata ya Lusu na kuwa na mshikamano,amani na umoja
baina ya wananchi hao.
DIWANI WA KATA YA LUSU WILAYANI NZEGA SAID MGALULA AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI WA IKULU FC KUBALA YA KUANZA KWA MTANANGE WA MGALULA CUP.
Alisema amefurahishwa
na namna ambavyo vijana wengi wanajitokeza katika kuonesha vipaji vyao hasa
kusakata kambumbu huku akiwasisitiza kila mmoja kutambua kipaji alichonacho na
kukindeleza.
“Napenda kuwahakikishia
kuwa leo mmetuburudisha vya kutosha sasa timu zote ambazo zipo kwenye kata
yangu nendeni mkaunde timu moja ya kata na mkisha kamilisha mchakato wa kupata
timu moja mtaniambia wakati huo tafuteni timu nyingine kutoka kata yoyote
ambayo mnaweza kushindana nami ntafadhili mchezo huo kwa kutoa zawadi kwa
mshindi.
Aidha katika mchezoa
ambaoumetoa mshindi wa jumla umezikutanisha timu za Isanga na Ikulu ambapo
Isanga iliibuka kwa ushindi wa Gori mbili Kwa moja.
Aidha katika mcheo huo
mchazaji machachali kabisa kulwa ngudungi aliipatia bao la uongozi Isanga FC
dakika ya 13 ya mchezo kwa shuti kali
liliomshinda mlinda lango wa Ikulu FC ambapo kipindi cha Pili timu zote
ziliingia kwa tahadhali kubwa lakini kutokana aina ya mchezo ulivyokuwa Ikulu
FC ilitawala mchezo kwa asilimia kubwa na hatimae kupata Gori la kuzawazisha
dakika ya 67 ya mchezo huku Isanga Fc nao wakarudi kwa kushambulia kwa kasi
kubwa ambapo dakika ya 71 Benjamin Charles akawapatia bao la uongozi Isanga FC.
Toka dakiki ya 71 timu zote zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu lakini hiyo haikutosha Isanga FC kuibuka kidedea na kutwaa ubingwa wa Mgalula cup.
Katika mashindano hayo
msindi wa kwanza amejinykulia kitita cha laki moja na nusu,150,000/ huku
mshindi wa pili akijipatia 100,000/ huku mshindi wa tatu akiwajipatia 50,000/
……….