WANUFAIKA BOMBA LA MAFUTA WAMSHUKURU RAIS SAMIA.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Naitapwaki Tukai akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi nyumba kwa mguswa wa bomba la mafuta Kata ya Mwangoye.
NA ODACE RWIMO, NZEGA DC
BOMBA la mafuta ni mradi mkubwa unaotekelezwa na serikali ya
awamu ya sita kutoka Hoyima Nchini Uganda hadi Mkoani Tanga nchini Tanzania
ambapo Bomba hilo hupita kwenye baadhi ya makazi ya watu.
Katika Mkoa wa Tabora Kata ya Mwangoye Wialayani Nzega , ni
miongoni mwa kata ambazo Bomba hilo limepita katika makazi ya watu ambapo
wamelazimika kuhama kupisha mradi ili
uweze kutekelezwa pasipo kuwa na kikwazo.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi Nyumba kwa
Mwananchi Mmoja wapo aliyepisha Mradi wa Bomba la Mafuta Mkuu wa wilaya ya Nzega
Mkoani hapa Naitapwaki Tukai alisema serikali italinda na kutunza haki za
wananchi wake wote ambao wamepisha mradi kuhakikisha wanapata fidia stahiki kwa
wakati.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai Akiwa na waguswa wa Bomba la Mafuta Hamis Mayaya na familiya yake na wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Bomba la mafuta Mkoani Tabora David kilala.
Alisema tayari karibia walengwa wote ambao waliahtirika kwa
namna moja ama nyingine kupitia mradi wa Bomba la mafuta tayari wameishatambuliwa
na kulipwa fidia huku wengi wao wakijengewa nyumba za kisasa kulingana na
nyumba walizokuwa nazo hapo awali.
Alisema serikali itaendelea kutunza haki za raia wake
kuhakikisha hawapati athali yoyote kwa kupisha mradi huo mkubwa unaotekelezwa na
serikali kwa manufaa ya nchi na ustawi wa Jamii ikiwa ni pamoja na kutunza mazingira ambayo mradi huo utapita.
“Unajua hii nyumba tunayokabidhi leo ni miongoni mwa nyumba 29 ambazo zimejengwa kwa watu ambao walipitiwa
na mradi ambao kimsingi hawakupenda kulipwa fedha taslim badala yake waliomba
kuboreshewa makazi yao kwa kujengewa nyumba za kisasa”alisema Tukai.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa Bomba la Mafuta Mkoani
Tabora David kilala alisema wamejipanga kuhakikisha wanatunza mazingira na
kulipa fidia kwa kila aliyeguswa na mradi huo kwa kuzingitia misingi ya haki na
utawala bora bila ya kumpunja mtu yeyote aliyekubali kwa hiari yake kupisha
mradi huo.
Alise ma si jambo ndogo mtu kuhama makazi yake aliyoyazoea na
kuhamia sehemu nyingine kwa ajili ya kupisha mradi wanapaswa kupongezwa kwa
moyo wa uzalendo walio uonesha kwa kujali masrahi mapana ya nchi yetu bili ya kujali masrahi
yao binafsi.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Naitapwaki Tukai akikagua nyumba iliyokabidhiwa kwa mguswa wa bomba la mafuta hamis Mayaya aliyevalia Tishti ya yanga.
Kilala alisema Mkoa wa Tabora wamejipanga kuhakikisha mradi
huo unatekelezwa kwa asilimia 100 kwa kiwango cha kimataifa bila ya kupoteza
rasilimali za Taifa hilo litaendana na utunzaji wa mazingira sanjari na utoa wa
elimu juu ya kutunza miradi ambayo inayotekelezwa mkoani hapo.
Alisema serikali ya Mkoa wa Tabora itahakikisha kila kitu
kinaenda kwa utaratibu uliopangwa kwa kushirikisha jamii yote inayopitiwa na
mradi huo hatua kwa hatua ikiwa ni pamoja na utoaji wa ajira kwa vijana ambao
wanasifa za kupata kazi kwenye maeneo ambayo Mradi wa Bomba la Mafuta linapita.
Naye Hamis Mayaya ambaye ni Mmoja wa waguswa wa mradi wa Bomba la Mafuta alimshukuru rais Samia Suluhu Hassan Kwa moyo wa kizalendo hasa kwa kuwajali watanzania Wote bila kujali anamaisha ya aina gani.
Alisema kitendo cha Serikali kufanya Tathimini kwa usahihi na
kutambua wajibu wa Raia wao wote na kuwapatia Stahiki zao kwa kupisha bomba la
mafuta limewatia moyo kuwa serikali inawajibika ipasavyo kwa wananchi wake hivyo inaonesha jinsi gani wamejipanga katika kutetea na
kulinda haki za raia.
Nyumba alizojengewa mguswa wa Bomba la mafuta Hamis Mayaya mkazi wa kata ya Mwangoye wilayani Nzega mkoani Tabora.
“Unajua ninyo furaha kubwa sana kumpongeza Rais Samia kwani
sikuwa na ndoto kama ningepata nyumba nzuri saana kama hii ambayo leo
nimekabidhiwa na wasimamizi wa bomba la mafuta ki ukweli kama ningepewa fedha ningekuwa
nimeisha imaliza pasipo kufanya jambo la maana”alisema Mayaya.
Hata hivyo alisema wataendelea kuiunga mkono serikali katika
miradi yote inayoendelea kutekelezwa mokani Tabora na kutunza hali ya usalama
na mzangira ikiwa ni njia mojawapo ya Kumuunga Mkono Rais Wa Jamuhuri Ya
Muungano wa Tanzania .